Julai 28, 2018

undani wa kupatwa kwa mwezi  na matokeo ya mwezi mwekundu.

Kupatwa kwa mwezi kutaanza polepole mwendo wa saa mbili na robo saa za Afrika mashariki na inatarajiwa kwamba raia wa Tanzania na wenzao wa Kenya wataweza kuliona tukio hilo la kihistoria ambalo litakuwa la muda mrefu zaidi katika karne ya 21.
Mwezi utaanza kupatwa muda huo huku ukipatwa kamili mwendo wa saa nne na nusu ambapo utabadilika na kuwa mwekundu.

Kutoka saa nne na nusu Tukio hilo litaendelea kwa dakika 51 ambapo kukamilika kwa tukio hilo la kihistoria kutaanza na baadaye kuendelea hadi saa sita na dakika 13 ambapo litakwisha.


Tukio hilo litakuwa la muda mrefu zaidi katika karne ya 21, kulingana na shirika la usimamizi wa anga za juu(NASA).
Na iwapo una bahati utafanikiwa kuona tukio hilo kwa saa moja na dakika 43.
Je kupatwa kwa mwezi ni nini?
Kupatwa kwa mwezi hutokea wakati jua, dunia na mwezi zinapokua kwenye mstari mmoja.
Hii inamaanisha kwamba dunia iko katikati ya jua na mwezi hatua inayoziba mwanga wa jua.

Kupatwa huko hutokea wakati mwezi unapoingia katika kivuli cha dunia.
Katika awamu tofauti kupatwa huko kwa mwezi kutafanyika kwa saa tatu na dakika 55.usiku.

Kwa nini unaitwa 'mwezi wa mwekundu'?

Usiku wa kupatwa kwa mwezi hushirikishwa na dhana na wa kuwepo kwa 'mwezi wa damu' kutokana na rangi yake nyekundu.
Hilo linatokana na athari za kutazama miale ya jua katika anga na rangi za machungwa na nyekundu zinazoonekana katika mwezi.

Ni lini na wapi utaonekana?
Kupatwa kwa mwezi mnamo tarehe 27 Julai kutaonekana Ulaya, Afrika, mashariki ya kati , katikati mwa Asia na Australia ikiwa ni maeneo yote isipokuwa kaskazini mwa Marekani.
Hautalazimika kutumia darubini kuutazama mwezi huo.

Nani atakayeuona vizuri zaidi?

Eneo zuri la kulitazama tukio hilo ni eneo nusu ya Mashariki mwa Afrika ,Mashariki ya kati na katikati mwa bara la Asia.
Tukio hilo halitaonekana katika maeneo ya kati na Marekani Kaskazini.
Kusini mwa Marekani , unaweza kuonekana kiasi katika maeneo ya mashariki hususan miji ya Buenos Aires, Montevideo, Sao Paulo na Rio de Janeiro.
Katika miji mingine ya karibu utaonekana wakati mwezi utakapokuwa ukiondoka katika eneo hilo-huo ni mstari ambao ardhi na anga zinaonekana kukutana.

Kivuli cha tukio hilo kitaonekana katika satelaiti bila kuziba mwangaza wote.
Nchini Uingereza hautaweza kuona mwanzo wa tukio hilo, hiyo ni kwa sababu mwezi utakuwa chini ya upeo wa macho.

Julai 13, 2018

Waasi wakubali matokeo Syria


Majengo katika mji wa Deraa yaliyoathiriwa na vitaVikosi vya Syria vimefanikiwa kurejesha udhibiti wa mji wa Deraa, uliokuwa unashikiliwa na waasi, eneo hilo ndipo mahala alikozaliwa rais wa taifa hilo Bashar al-Assad.Waaasi hao wamekubali kuweka silaha chini.

Waliingia katika eneo hilo na kufanikiwa kupandisha bendera ikiwa ni alama ya kujitangazia udhibi wa mji huo. Waasi wamearifu kuwa wamearifu kusalimu amri na kuelekea katika eneo la kaskazini ambalo ni salama kwao.
Hata hivyo majeshi hayo ya serikali pia yamefanikiwa kukamata magari ya waasi hao na mali nyingine ambazo walikuwa wakizitumia tangu walishikilie eneo hilo june 19 mwaka huu.
Umoja wa mataifa unasema kuwa watu wapatao maelfu ya raia waliokuwa wamepewa hifadhi katika mpaka wa Jordan wamerejea katika makazi yao,kufuatia waasi kusalimu amri na kukubali kuweka silaha chini hapo jana na kukubaliana na serikali. Mji huo una umuhimu mkubwa,kwani ,ni jimbo ambalo lililopo na Jordan,na ndipo zilipoanzia harakati za upinzani mwezi machi mwaka 2011.

Agosti 07, 2017

ALIYO YASEMA KENYATA KABLA YA UCHAGUZI KENYA

Rais KenyattaHaki miliki ya pichaKenyatta ametoa hotuba yake ya mwisho kabla ya uchaguzi mkuu Jumanne
Rais Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa wapiga kura nchini humo kuondoka kwenye vituo vya kupigia kura na kwenda nyumbani baada ya kupiga kura.
Kiongozi huyo, katika hotuba kwa taifa kabla ya uchaguzi mkuu Jumanne, amesema wananchi wanafaa kupiga kura kwa amani.
"Ombi langu ni kwamba tunapopiga kura, hebu tupige kura kwa amani na tukumbuke kama nilivyosema jana, kwamba baada ya kupiga kura yako, nenda nyumbani. Nenda kwa jirani yako," amesema.
"Bila kujali anatoka wapi, kabila lake, rangi au dini, jirani yako ni ndugu yako. Jirani yako ni dadako.
"Jinsi ulivyopiga kura haifai kwa vyovyote vile kuathiri au kubadilisha jinsi unavyohusiana na jirani yako.
"Msalimie kwa mkono, kuleni chakula pamoja na uwaambie 'hebu tusubiri matokeo' kwani Kenya itaendelea kuwepo kwa muda mrefu hata baada ya uchaguzi."
Muungano wa upinzani ulikuwa awali umewashauri wafuasi wake kutoondoka vituo baada ya kupiga kura 'kulinda kura'.
Lakini baadaye, muungano huo ulibadilisha wito wake na kuwashauri waondoke baada ya kupiga krua lakini warejee baadaye jioni.
Polisi wamewataka wananchi kuheshimu sheria ya kutokuwa karibu na vituo vya kupigia kura umbali wa mita 400 baada ya kupiga kura.
"Wazazi wetu walipigana ndipo tuwe na Kenya nzuri na maisha mazuri…bila kujali matokeo ya uchaguzi huu, ni lazima tuendelee kushikamana pamoja kama wananchi. Zaidi ya yote, tukatae kutishwa. Lazima tukatae ghasia au majaribio yoyote ya kutugawanya," amesema Bw Kenyatta.

Julai 11, 2017

  1. UNDANI WA KURUDISHWA FEDHA ZA ESCROW SHILINGI MILIONI 40.4

TanzaniaHaki miliki ya pichaGOOGLEImage caption
1. Kama inavyokumbukwa, kutokana na ukweli kwamba ilisharipotiwa sana kwenye vyombo vya habari, kwamba tarehe 12/02/2014 nilipokea fedha kiasi cha shilingi milioni 40.4 za kitanzania kutoka kwa Ndugu James Rugemalira, mmiliki wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd. Fedha hizo nilizipokea kupitia akaunti yangu namba 00110102352601 ya Benki ya Mkombozi.
2. Fedha hizo nilizipokea, kwa nia njema, kama msaada/mchango kutoka kwa ndugu Rugemalira ili zinisaidie katika kutimiza majukumu yangu ya kibunge, hususan,kusaidiana na wananchi wa jimbo langu la Sengerema na Taifa kwa ujumla, kutekeleza shughuli za kijamii (mfano ujenzi wa makanisa, misikiti, kusaidia kulipia karo za wanafunzi wasiojiweza, n.k) na shughuli za miradi ya maendeleo ambayo haipo kwenye bajeti ya serikali.
3. Nilipokea Fedha hizo kutoka kwa ndugu Rugemalira bila kujua kwamba fedha hizo zilikuwa zinahusishwa na kashfa ya akaunti ya fedha za Escrow kama ilivyo sasa.
4. Fomu ya Tamko langu kama kiongozi wa umma kuhusu rasilimali na madeni kwa mujibu wa sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 kwa kipindi kilichoishia 31 Desemba, 2014, niliyoiwasilisha ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma tarehe 24/12/2014 ilijumuisha msaada huu wa shilingi milioni 40.4 kutoka kwa ndugu James Rugemalira.
5. Tarehe 15/01/2015 nililipa kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kiasi cha Shilingi 13,138,125/= ikiwa ni sawa na asilimia 30 (30%) ya msaada huo niliopewa, kama ilivyoelekezwa na TRA.

TanzaniaHaki miliki ya picha
Image captionWilliam Ngeleja akifafanua jambo mbele ya Wanahabari

SABABU ZA KURUDISHA FEDHA HIZI.
i) Nilipokea msaada huu kama wapokeavyo wabunge wengine, kwa nia njema, bila kujua kwamba James Rugemalira baadaye angekuja kuhusishwa na kashfa ya fedha za akaunti ya ESCROW kama ilivyo sasa.
ii) Kwa vile sasa imedhihirika kwamba aliyenipa msaada huu anatuhumiwa kwenye kashfa ya akaunti ya ESCROW, nimepima na kutafakari, na hatimaye nimeamua, kwa hiari yangu mwenyewe, kurejesha serikalini (TRA) fedha zote nilizopewa kama msaada (TZS milioni 40.4) bila kujali kwamba nilishazilipia kodi ya mapato kama nilivyoeleza hapo awali. Risiti ya ushahidi wa kurejesha fedha hizi serikalini hii hapa.
iii) Nimeamua kurejesha fedha hizi hata kama aliyenipa msaada bado ni mtuhumiwa tu, kwa vile hajathibitika kupatikana na hatia, kwa sababu sitaki kuwa sehemu ya kashfa/tuhuma hizo.
iiii) Leo nina zaidi ya miaka 12 nikiwa kiongozi wa Umma, na pia niliwahi kuitumikia wizara ya Nishati na Madini kwa takribani miaka mitano na nusu ( Naibu Waziri/Waziri), lakini sijawahi kukumbwa na kashfa ya rushwa au ufisadi. Kwa hiyo nimesononeka na kufadhaika sana kuona kuwa msaada niliopewa sasa unahusishwa na tuhuma.
v) Ninarudisha fedha hizi ili kulinda heshima na maslahi mapana ya nchi yangu, chama changu (CCM), Serikali yangu, Jimbo langu la Sengerema, familia yangu na heshima yangu mwenyewe.
HITIMISHO
• Kupokea msaada ni jambo la kawaida, ila ikibainika kuwa msaada unaopewa una harufu ya uchafu hata kama haujathibitishwa na vyombo husika ni vyema kujiepusha nao.
• Ninampongeza, kwa dhati kabisa, Rais wetu mpendwa Dr John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya kwa maslahi ya Taifa letu. Nami naungana na watanzania wenzangu wazalendo kumuombea kwa Mungu na namhakikishia nitaendelea kumuunga mkono kwa kupigania maendeleo ya nchi yetu.
BBCSWAHILI


Watu 16 wafariki kwenye ajali ya ndege Marekani


A still image showing a crashed plane in flames in a field, taken from video footageHaki miliki ya pichaSIma
Takriban watu 16 wamefariki kwenye ajali ya ndege ya jeshi kwenye jimbo la Mississipi nchini Marekani.
Ajali hiyo ilitokea katika kaunti ya LeFlore karibu kilomita 160 kusini mwa mji mkuu wa jimbo hilo, Jackson.
Watu wote 16 waliokuwa ndani ya ndege hiyo waliangamia.
Hakuna taarifa rasmi zilizotolewa kuhusu kilichosababisha kutokea ajali hiyo.
Kwa mujibu wa jarida la jimbo la Mississipi ni kuwa ndege hiyo ilianguka katika shamba moja na mabaki yake yakatabakaa mbali.
A BBC map showing Leflore County in Mississippi stateBBCSWAHILI

Trump Junior atetea mkutano na wakili wa Urusi aliyedai kuwa na taarifa kumhusu Hillary Clinton


Donald Trump Jr at Trump Tower in New York City, 18 January 2017Haki miliki ya picha
Image captionTrump Jr anasisitiza kuwa wakili huyo hakutoa taarifa muhimu kumhusu Bi Clinton
Mtoto wa kiume wa rais wa Marekani Donald Trump amevishambulia vyombo vya habari kufuatia madai ya mkutano na wakili mrusi ambaye alisema kuwa alikuwa na habari za kumchafulia jina Hillary Clinton.
Donald Trump Jr amekana kutoa habari za kukanganya kuhusu mkutano huo wa mwaka uliopita.
Pia amesema kuwa lilikuwa jambo la kawaida kupata taarifa kuhusu wagombea pinzani.
Maafisa nchini Marekani wanachunguza madai yanayohusu Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani.
Mkwe wa Trump Jared Kushner na aliyekuwa mkuu wa kampeni Paul J Manafort, walikuwa pia katika mkutano huo na Natalia Veselnitskaya.
Haki miliki ya pichaImage caption
Trump Jr anasisitiza kuwa wakili huyo hakutoa taarifa muhimu kumhusu Bi Clinton, ambaye alikuwa mshindani wa babake katika kiti cha urais.
Mkutano huo ulifanyika tarehe 9 mwezi Juni mwaka 2016 katika jengo la Trump Tower, wiki mbili baada ya Donald Trump kupata uteuzi wa Republican.
Unaaminiwa kuwa mkutano wa kwanza wa siri kati ya raia wa Urusi na watu waliokuwa karibu na Bwana Trump.
Baada ya New York Times kuripoti mara ya kwanza kuhusu mkutano huo siku ya Jumamosi, Bwana Trump Jr alitoa taarifa iliyothibitisha kuwa mkutano huo ulifanyika lakini haikutaja ikiwa ulihusu kampeni ya kuwania urais
BBCSWAHILI

Juni 19, 2017

Marekani yaidungua ndege ya Keshia la Syria.

Marekani Yaidungua ndege ya kijeshi ya Syria


US F/A-18E Super HornetHaki miliki ya picha

Image captionMuungano unaoongozwa na Marekani nchini Syria umeangusha ndege ya jeshi la Syria katika mkoa wa Raqqa.

Jeshi la Syria lilisema kuwa ndege yake ya kijeshi ilikuwa katika harakati za kushambulia kundi la Islamic State wakati ilishambuliwa siku ya Jumapili.
Imesema kuwa kisa hicho kitakuwa cha athari katika vita dhdi ya ugaidi.
Marekani ilisema kuwa ilichukua hatua za kujilinda baada ya serikali ya Syria kuangusha mabomu karibu na wapiganaji wanaoungwa mkono na Marekani.
Kisa hicho kilitokea mji wa Ja'Din ambao unashikiliwa na vikosi vya Syrian Democratic Forces (SDF).
Wapiganaji wa SDF wanaoungwa mkono na muungano unaoongozwa na Marekani wamezingira ngome ya IS huko Raqqa.
Saa mbili kabla ya ndege hiyo kuangushwa, Marekani ilisema kuwa vikosi watiifu kwa raisi wa Syria Bashar al-Assad viliwashambulia wapiganaji wa SDF na kuwajeruhi kadha.
Mapema mwezi huu, Marekani iliangusha ndege isiyo na rubani ya seriikali ya Syria, baada ya ndege hiyo kushambulia vikosi karibu na kivuko cha mpaka cha al-Tanf kwenye mpaka kati ya Syria na Iraq.
BBCswahili.