Waasi wakubali matokeo Syria

Waliingia katika eneo hilo na kufanikiwa kupandisha bendera ikiwa ni alama ya kujitangazia udhibi wa mji huo. Waasi wamearifu kuwa wamearifu kusalimu amri na kuelekea katika eneo la kaskazini ambalo ni salama kwao.
Hata hivyo majeshi hayo ya serikali pia yamefanikiwa kukamata magari ya waasi hao na mali nyingine ambazo walikuwa wakizitumia tangu walishikilie eneo hilo june 19 mwaka huu.
Umoja wa mataifa unasema kuwa watu wapatao maelfu ya raia waliokuwa wamepewa hifadhi katika mpaka wa Jordan wamerejea katika makazi yao,kufuatia waasi kusalimu amri na kukubali kuweka silaha chini hapo jana na kukubaliana na serikali. Mji huo una umuhimu mkubwa,kwani ,ni jimbo ambalo lililopo na Jordan,na ndipo zilipoanzia harakati za upinzani mwezi machi mwaka 2011.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni