Desemba 31, 2016

Kuna uwezekano wa Ibrahimovic kuvunja rekodi ya Messi kabla msimu huu kuisha.


Moja kati ya usajili ambao ulishangaza baadhi ya watu kuona unafanyika ni Man Unitedkumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden Zlatan Ibrahimovic akiwa na umri wa miaka 35 kama mchezaji huru akitokea Paris Saint Germain ya Ufaransa katika kipindi cha dirisha la usajili la majira ya joto.
Wengi hawakutegemea kuona Zlatan akifanya vizuri na Man United kutokana na umri wake halafu alikuwa anaingia Ligi mpya, hivyo inaaminika angeweza kuchelewa kufanya vizuri au kushindwa kabisa, ila Zlatan amekuwa na mchango mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya Man United na leo anaweza kuvunja rekodi ya Lionel Messi.
screen-shot-2016-12-31-at-8-14-03-am
List ya washindi wanaoongoza kwa ufungaji magoli mengi kwa mwaka 2016
Zlatan anaweza kuvunja rekodi ya Messi ya kufunga magoli 51 kwa mwaka 2016 kabla mwaka haujaisha, kwani Zlatan  kafunga magoli 50 kwa mwaka 2016 kama akifunga goli mbili katika mchezo wa leo dhidi ya Middlesbrough anaweza kuvunja rekodi ya Messikwa kufikisha magoli 52 wakati huu ambao Ligi ya Hispania imesimama.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni